User Rating: 5 / 5

Star ActiveStar ActiveStar ActiveStar ActiveStar Active
 

SALA YA KUOMBEA SINODI YA MAASKOFU:

Tunasimama mbele yako ewe Roho Mtakatifu

Tunapokusanyika pamoja kwa jina lako

Wewe pekee unayetuongoza

Weka masakani yako ndani ya nyoyo zetu;

Utufundishe njia ya kupita na jinsi ya kuenenda

Sisi ni dhaifu na wenye dhambi

Usiruhusu tuendelee kuchochea machafuko.
Usiruhusu ujinga utuongoze kwenye njia mbaya

Wala utepetevu usiathiri matendo yetu
Utuwezeshe ndani yako tuwe na umoja
Ili tuweze kusafiri pamoja hadi uzima wa milele,

Wala tusipotee mbali kutoka njia ya kweli na iliyo sahihi,

Tunaomba yote hayo kwako wewe ufanyae kazi kila mahali na kila wakati,

Katika ushirika wa Baba na Mwana, milele na milele.

Amina.