UTARATIBU WA KADI ZA VALENTINE DINNER

1. Kila kikundi kinapaswa kuuza kadi na kupeleka pesa ofisini na kuchukua risiti kama ilivyo desturi yetu.

2. Sherehe hii sio ya wanandoa pekee ila Kila mmoja anaruhusiwa. Unaweza kuja na rafiki, ndugu, dada, mfanya kazi mwenzako n.k vile vile kadi za singles pia zinapatikana ofisini.

3. Unaweza kuuza kadi za valentine dinner kwa marafiki hata wasio waumini wa kathedrali.

4.. Mwisho wa ukusanyaji wa pesa za kadi ni tarehe 6/2/2023.

5. Kadi tayari zipo ofisini na VIONGOZI wameanza kuzichukua. Kadi hizi hazirudishwi kwani tunaendelea na misururu ya kutafuta pesa za kuanza ujenzi wa jumba la sentinari huku tukiburudika.

6. Wanandoa wanaotaka kukiri upya ahadi zao za ndoa wanaombwa kujisajili kabla ya tarehe 31/1/23 bila malipo yoyote ya ziada. WhatsApp group ya wanandoa hao itafunguliwa ili kufanikisha matayarisho.

Ujumbe huu umeletwa kwa niaba ya kamati ya mipango HGC.